Skip to main content

JAJI SIYANI AJITOA KUSIKILIZA KESI YA MHE: MBOWE NA WENZAKE .


Jaji Kiongozi Mustapha Siyani, amejiondoka kusikiliza kesi ya uhujumu inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mwenzake.


Jaji Siyani amesema sababu ya kujitoa kusikiliza kesi hiyo ni kutokana na  majukumu aliyoyanayo ambayo ameona yanaweza kumfanya ashindwe kuendesha kesi kwa haraka.


Uamuzi wa kujiondoa kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 16/2021, ameutoa leo, Oktoba 21, 2021 mara baada ya kutoa uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mbowe na wenzake. 



Jaji Siyani anakuwa wa pili kujitoa baada ya Septemba 6, mwaka huu Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, kujitoa kusikikiza kesi ya Mbowe na wenzake. 


Uamuzi wa kujitoa Jaji Luvanda kusikikiza kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021, ulitokana na Mbowe kwa niaba ya wenzake kuwa hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.


Mbowe alitoa madai hayo Jumatatu ya Septemba 6, 2021 muda mfupi baada ya Jaji Luvanda kutupilia mbali mapingamizi mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa mahakamani hapo dhidi ya washtakiwa hao.


Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama ya kutenda kosa na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya ugaidi.

Comments

  1. nani anataka kutoa hukumu ya kesi isio ya kweli hakuna zambi mbaya kama hiyo
    bibilia inasema usimshuhudie jirani yako uongo hongera jaji Siyani

    ReplyDelete

Post a Comment