Baada ya Future na Drake, sasa French Montana na Fetty Wap kuja na mixtape yao!

Baada ya Future na Drake kufanya kazi kwa pamoja na kuachia mixtape iliyopewa jina‘What A Time To Be Alive’, wasanii wengine wa Hip Hop wameona sio mbaya wakifuata ramani ya Future na Drake.
Rapper French Montana na Fetty Wap wamekuwa wakishirikiana kwenye nyimbo nyingi kipindi hiki na kwa mujibu wa kaka yake French Montana na mkurugenzi wa lebo yaCoke Boys MusicZack.. taarifa ikufikie kwamba wawili hao wapo studio kutengeneza mixtape yao mpya iliyopewa jina ‘Coke Zoo’.
coke boys
French Montana na Fetty Wap wakiwa na Zack Mkurugenzi wa lebo ya Coke Boys Music inayomsimamia French Montana.
>>> “Kwa sasa mixtape hiyo itakuwa na nyimbo saba, moja nikiwa nimeshirikishwa pia, na baadhi ya single zimewekwa online pia…” <<< alisema Zack Mkurugenzi wa Coke Boys Music.
Wakati tukiwa tunaendelea kusibiri ujio wa mixtape hiyo kutoka kwa French Montana naFetty Wap, nimeona itakuwa poa kama nikishare na wewe single yao iliyotoka hivi kariuni‘Freaky’… Kama ilikupita na mpaka sasa hujaisikia basi karibu ukisikilize hapa chini mtu wangu.

Comments