Fetty Wap kaivujisha hii mpya na anataka ikufikie; ‘In My Ways’
Fetty Wap - In My Ways
Licha ya kupata ajali ya pikipiki, msanii wa muziki wa HipHop Marekani, Fetty Wap ameona hana sababu ya kuacha kutengeneza muziki na kutupa burudani… wiki iliyopita msanii huyo mwenye hit single yake ya ‘Trap Queen’ aliisogeza kwetu mixtape yake na French Montana iliyopewa jina Coke Zoo, na sasa staa huyo amerudi tena kuziweka headlines kenye kurasa za burudani.
Kama wewe ni shabiki wa muziki wa HipHop na Fetty Wap basi hii good news ikuguse popote ulipo mtu wangu, siku ya Alhamisi wiki hii Fetty Wap ambaye pia ni kiongozi wa kundi lake la muziki la Zoo Gang aliamua aivujishe single yake mpya iliyopewa jina ‘In My Ways’.
Inawezekana single hii imeshagusa
masikio yako tayari lakini kama bado hujafanikiwa kukutana nayo basi
karibu uisikilize single hiyo kwa mara ya kwanza hapa chini mtu wangu.
ys (prod by. Peoples X Shy)
Comments
Post a Comment