Kila wiki Ty Dolla $ign atoa single mpya, wiki hii anaisogeza; ‘Sitting Pretty’ feat. Wiz Khalifa
Rapper na Producer Ty Dolla $ign amekuwa akiziandika headlines za burudani kila mwisho wa wiki kwa kuachia single mpya kuelekea uzinduzi wa Album yake mpya Free TC, inayotegemea kuwa sokoni Tarehe 13 November 2015… wiki hii je?
Baada ya kuziandika headlines ijumaa iliyopita kwa kuachia video mpya, ‘Solid’ alioshirikiana na msanii mkongwe wa R&B Marekani, Baby Face… wiki hii Ty Dolla $ign amerudi na single mpya ambayo ndani mkali mwengine wa HipHop, Wiz Khalifa kashirikishwa.
Wimbo unaitwa ‘Sitting Pretty’, na single hii ni miongoni wa nyimbo zinazobeba Album mpya ya Ty Dolla $ign Free TC. Wasanii wengine watakaosikika kwenye Album mpya ya msani huyo ni pamoja na Kanye West, Kendrick Lamar, Brandy, Trey Songz, P Diddy, R. Kelly, Future na wengine kibaO
Comments
Post a Comment