MATUKIO YA UKEKETAJI YAENDELEA HANANG’
MATUKIO ya vitendo vya ukatili vya uekeketaji bado vimeshamiri Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, ambapo inadaiwa asilimia 90 ya wanawake wa eneo hilo wamefanyiwa ukeketaji. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwa vitendo vya ukeketaji wa wanawake ikiwemo, kuzimia, fistula, kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua mtoto, kuzimia, kupata uambukizo (Infection), kuambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) na kupata Tetanus. Madhara mengine ni maumivu ya Kisaikolojia, maumivu wakati wa kukojoa, kuziba kwa njia ya mkojo, kuchanika vibaya wakati wa kujifungua, maumivu ya kisaikolojia, kuchelewa kujifungua na kifo. Hata hivyo, baadhi ya wananchi wanatupa lawama zao kwa taasisi zinazohusika na haki za wanawake na watoto kwani wanakaa maeneo ya mjini huku vijijini vitendo hivyo vikiendelea kushamiri kutokana na ukosefu wa elimu hiyo. Kwenye wilaya ya Hanang’ zaidi ya asilimia 90 ya wanawake wamefanyiwa ukeketaji huku polisi wakiendesha zoezi la kuw...