WAKURUGENZI WATAKIWA KUTOA TAARIFA KUHUSU MADAI YA WALIMU




WAKURUGENZI WATAKIWA KUTOA TAARIFA KUHUSU MADAI YA WAKIMU

…………………………………………….
Wakurugenzi wa Jiji, Manispaa, Miji pamoja na Halmashauri za Wilaya watakiwa kuandika barua kwa walimu ambao madai yao yalikataliwa au kupunguzwa ili kuwapa taarifa sahihi kuhusu madai hayo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini dare s salaam kuhusu madai na madeni ya watumishi wa umma.
Bw. Mkwizu amesema kuwa Serikali imekuwa ikishughulikia madai na madeni ya watumishi wa umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazotawala utumishi wa umma.
“Madai na madeni ya watumishi wa umma yamegawanyika katika makundi mawili, madai yanayohusu mshahara ambayo hutokana na mtumishi kuchelewa au kutokurekebishiwa mshahara pindi apandishwapo cheo pamoja na madai yasiyohusu mshahara ambapo mwajiri huchelewa kulipa gharama za likizo, masomo matibabu na uhamisho” alifafanua Bw. Mkwizu.
“Kwa upande wa walimu Serikali imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ili kuweza kufanikisha ulipaji wa madai ya walimu na hii haimaanishi kuwa madeni ya watumishi wengine yamesahaulika” aliongeza Bw. Mkwizu.
Aidha, walimu wapatao 45,453 wanamadai ya malimbikizo ya mshahara ya shilingi 32,104,487,430, hadi kufikia Septemba mwaka huu Serikali imewalipa walimu 3,379 jumla ya shilingi 2,387,451,410 na walimu wapoatao 1,667 wenye madai ya shilingi 1,733,641,362.7 watalipwa mwezi huu wa octoba, alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo.
Hata hivyo pamoja na jitihada zilizofanyika za kuboresha Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Walimu baadhi ya waajiri hawajatekeleza kikamilifu muundo huo hivyo wametakiwa kutoa kipaumbele kwa kuwapandisha madaraja walimu wapatao 41,700 waliogota katika muundo uliopita.

Comments