Kingunge vs. CCM, Dk. Slaa kwa Magufuli, Rais wa Nigeria kusimamia Uchaguzi Tz? Kagame? Nchemba je?

Kingunge azidi kuipasua CCM, Dk. Slaa asema Magufuli ndio chaguo sahihi, Lowassaavunja rekodi Arusha,  Rais wa Nigeria kusimamia Uchaguzi Mkuu October 25!?
Rais wa Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari na Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi wanatarajia kuja kusimamia Uchaguzi Mkuu October 25 wakiwa miongoni wa waangalizi 600 kutoka umoja wa EU… DkJohn Magufuli ampigia debe Mrema Mkoa wa Kilimanjaro asema kuwa itakuwa ni dhambi kumchagua mtu ambae haijui vizuri historia ya jimbo la Vunjo kama yeye.
Kingunge apanda jukwa la UKAWA kumnadi mgombea Urais kupitia CHADEMAEdward Lowassa Arusha, aishambulia CCM asema haitoweza kuiongoza Serikali kwa awamu ya tano… Mchungaji Christopher Mtikila amezikwa jana katika kijiji cha Milomkoani Njombe.
Mgombea Ubunge Bunda Mjini kupitia CHADEMA Esther Bulaya alazwa mahabusu mjini Bunda kwa madai yakuwa yeye na wenzake walitaka kuvamia kituo cha Polisi, Mgombea huyo na wenzake kufikishwa Mahakamani leo.
Mwigulu Nchemba amewaonya watu wanaotumia vibaya maneno ya Baba wa TaifaMwl. Julius K. Nyerere, Mahakama yamsafishia njia Rais Paul Kagame na sasa kutawala kwa awamu ya tatu.

Comments